Mugabe: Ninaweza kukutwanga ngumi

Mugabe Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mugabe alianza kuhudumu muhula wa sasa 2013

Kiongozi wa muda mrefu wa Zimbabwe Robert Mugabe amejibu kwa mzaha swali kuhusu mrithi wake na kusema bado anaweza kurusha ngumi.

Rais Mugabe aliulizwa nani atakayemrithi wakati wa sherehe ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Kiongozi huyo ambaye amekuwa uongozini tangu 1980 ametimiza umri wa miaka 92.

"Mbona unamtaka mrithi?" alimwuliza aliyekuwa akimhoji.

“Unataka nikutwange ngumi uanguke chini ndipo uamini kwamba bado nina nguvu?”, gazeti la serikali ya Herald limemnukuu.

Bw Mugabe, alisema hatastaafu katikati mwa muhula wake wa sasa, ambao ulianza 2013.

“Mbona nikubali kuendelea kuongoza iwapo nina maradhi au ninaugua au siwezi kuongoza?” aliuliza.