Waliopanga ndoa ya mapema Pakistan wakamatwa

Image caption Ndoa za watoto nchini Pakistan

Polisi huko Mashariki mwa Pakistan wamewakamata watu wanne wanaotuhumiwa kupanga ndoa kati ya mvulana mwenye umri wa miaka 14 na msichana mwenye umri wa miaka 10 pekee, miaka ambayo inachukuliwa kuwa ya chini.

Zaidi ya hayo ni kuwa ndoa hiyo ilikuwa imepangwa kama njia ya kusuluhisha mzozo baina ya familia hizo mbili.

Baraza la wanakijiji wa eneo hilo lilikubali kuidhinisha ndoa hiyo baada ya kaka wa msichana aliyepangiwa kuolewa, kukabiliwa na tuhuma kwamba alimuua mkewe.

Tabia ya kuendeleza ndoa za mapema na vile vile kutatua mizozo ya kinyumbani kupitia ndoa, ni hatia kwa mujibu wa sheria za Pakistan.