Simon Wood alikuwa nani?

Wood Haki miliki ya picha PA
Image caption Wood alijiua baada ya kushtakiwa

Simon Wood alikuwa rubani wa shirika la ndege la British Airways aliyetuhumiwa kuwanyanyasa kingono watoto Afrika Mashariki. Alituhumiwa pia kuwanyanyasa kingono watoto Uingereza.

Alitoka Potters Bar eneo la Hertfordshire.

Alituhumiwa kuwanyanyasa kingono watoto akiwa ziarani Afrika akifanya kazi za kusaidia wasiojiweza katika jamii.

Aligongwa na gari moshi karibu na kituo cha treni cha Potters Bar tarehe 18 Agosti siku 11 kabla ya siku ambayo alitarajiwa kufika kortini. Alikuwa na umri wa miaka 54 wakati huo

Alikuwa ameshtakiwa Uingereza na kosa moja ya kunyanyasa msichana wa umri wa chini ya miaka 16, makosa mawili ya kumpiga mtoto piga za uchi na kosa moja ya kumiliki picha za uchi za mtoto.

Akiwa Afrika, alidaiwa kuwanyanyasa wasichana wa umri wa kati ya miaka mitano na 18 katika shule na vituo vya kuwatunza mayatima kati ya 2001 na 2013, mawakili wa Leigh Day walisema.

Mawakili hao waliishtaki British Airways wakisema ilifaa kulaumiwa kwa sababu waathiriwa walidhulumiwa Bw Wood akiwa ametua Afrika kikazi.

Wakati wa Pasaka 2002, Bw Wood alikuwa miongoni mwa wahudumu wa ndege 20 kutoka ndege mbili za British Airways waliojitolea kushiriki hafla ya kuwasaidia wasiojiweza katika jamii katika kituo kimoja cha kuwatunza mayatima.

Walijitolea kukaa kipindi hicho cha likizo na watoto hao na kutoa zawadi, dawa na misaada kwa kituo hicho cha mayatima.