Unyanyasaji wa kingono wazidi dhidi ya wanajeshi wa UN

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanajeshi walinda amani wa Umoja wa Mataifa

Madai ya unyanyansaji wa kingono dhidi ya wanajeshi walinda amani wa Umoja wa Mataifa yaliongezeka kwa thuluthi moja mwaka uliopita,kulingana na ripoti ya umoja huo.

Kulikuwa na madai 69 dhidi ya walinda amani mwaka 2015 kutoka 52 mwaka 2014 huku madai 66 yakitolewa mwaka 2013.

Thuluthi moja ya madai ya mwaka 2015 yalitolewa katika taifa la Afrika ya kati CAR.

Kwa mara ya kwanza ,ripoti hiyo pia imeziorodhesha nchi zote ambazo wanajeshi wake walihusishwa chini ya jina ''watajwe ili waaibike''.

Kwa jumla wanajeshi 10 walinda amani walidaiwa kufanya unyanyasaji 2015.

Madai hayo yanahusisha wanajeshi,polisi wa kimataifa maafisa wengine na waliojitolea.

Kulingana na takwimu mpya za umoja wa mataifa kuna takriban maafisa 124,746 wanaohudumu katika maeneo 16 mbali mbali duniani.