Ben Carson ajiondoa mchujo wa Republican

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ben Carson kushoto

Daktari Bingwa wa upasuaji wa ubongo, Ben Carson, ametangaza rasmi kuwa amejiondoa katika ugombezi wa kura za mchujo wa Urais katika chama chake cha Republican nchini Marekani.

Akiongea katika mkutano wa wanachama wa Republican wasiopendelea mabadiliko, Daktari Carson alisema alikuwa akiondoka kwenye kampeni.

Mwanzoni mwa kampeni hiyo alikuwa mstari wa mbele lakini kwa sasa ameondoka katika uchaguzi huo wa mchujo bila kushinda jimbo lo lote miongoni mwa 15 ambayo tayari yamefanya uamuzi wake.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ben Carson kulia akiwa katika mjadala wa chama cha Republican hapo awali.

Alikuwa mgombea ambaye alikuwa kifua mbele wakati kampeni zilipoanza lakini alifanya vibaya wakati wa kampeni akionyesha udhaifu katika maswala ya kigeni mbali na kudanganya kuhusu mizizi yake mbali na kulinganisha mradi wa Obama wa matibabu na utumwa.

Hatahivyo Carson hajasema ni nani kati ya wagombea wa nne wa Republican atakayemuunga mkono.