Masoko ya ng'ombe ya Boko Haram yafungwa

Haki miliki ya picha Nigeria Army
Image caption Soko la kuuza ngombe la Boko haram

Masoko manne ya ng'ombe ambayo ngombe za wizi zilikuwa zikiuzwa ili kufadhili kundi la wapiganaji la Boko haram yamefungwa.

Wapiganaji hao wamekuwa wakitumia maajenti kuuza ng'ombe zilizoibwa kulingana na gavana wa jimbo la Borno.

Haki miliki ya picha Nigeria Army
Image caption Soko la Boko Haram

Biashara ilisitishwa kwa kipindi cha wiki mbili katika soko la ngombe la Gamboru,ambalo ni miongoni mwa masoko makubwa Afrika.

Boko Haram limeiba ng'ombe wengi nchini Nigeria na taifa jirani la Cameroon.

Haki miliki ya picha Nigeria Army
Image caption Boko Haram

Mashambulio ya miaka sita ya kundi hilo yamesababisha vifo vya watu 17,000,kuharibu shule 1000 na kuwawacha zaidi ya watu milioni mbili bila makao.