Obama kuhamia Washington DC

Image caption Familia ya rais Obama kuhamia

Rais Barack Obama wa Marekani ataondoka katika ikulu ya White House mapema mwaka 2017, lakini hatahamia mbali.

Bwa Obama alisema siku ya Alhamisi kwamba familia yake itahamia mjini Washington, huku mwanawe wa kike Sasha akimaliza shule katika Elite Academy, Sidwel Friends.

''Kumhamisha mtu katikati ya mafunzo ni ngumu'', alisema alipokuwa akijibu maswali huko Wisconsin.

Si jambo la kawaida kwa marais kuishi katika mji mkuu baada ya kuondoka madarakani.

Woodrow Wilson ambaye alihudumu kama raia mwaka 1913 hadi 1921 alikuwa wa mwisho kufanya hivyo.

Hata hivyo familia ya Obama pia inapanga kuishi kwa muda mjini Chicago, ambapo familia ina nyumba na Bi Michelle Obama ana familia yake.

Obama pia anaimarisha maktaba yake mjini Chicago.