Makubaliano ya amani yaendelea kuafikiwa Syria

Haki miliki ya picha AFP Getty Images
Image caption Syria

Ni juma moja sasa tangu kusitishwa kwa mapigano ambayo yamepunguza sana uhasama nchini Syria.

Kulikuwa na matukio machache ya mashambulizi hayo siku ya ijumaa Mashariki mwa mji mkuu wa Damascus.

Lakini katika maeneo mengine mashirika ya kutoa misaada yaliendelea na shughuli zake za kutoa huduma za kibinadamu, hata katika maeneo matatu yanayoshikiliwa na waasi na kuvamiwa mara kwa mara na wanajeshi wa Serikali.

Mwandishi wa BBC wa Damascus ameongea juu ya hali ya utulivu katika maeneo hayo lakini akasisitiza kuwa raia wengi wa Syria hawaamini kuwa hali hiyo ya amani itadumu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mazungumzo ya amani kuhusu Syria

Mashauriano ya awali ya amani yanatarajiwa kuanza tena mjini Geneva juma lijalo.

Hata hivyo kundi kubwa zaidi la waasi limeeleza wasiwasi wake kuwa huenda lisihudhurie mkutano huo.