Tottenham yatoka sare na Arsenal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsenal dhidi ya Tottenham

Alexis Sanchez alisawazisha na kuifanya timu yake iliokuwa na wachezaji 10 uwanjani kupata pointi moja huku timu ya Tottenham Hotspurs ikikosa fursa muhimu ya kupanda katika uongozi wa jedwali la ligi.

Bao la Aaron Ramsey liliiweka mbele Arsenal kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Kiungo wa kati wa Arsenal Francis Coquelin alipewa kadi nyekundu baada ya dakika 55 alipomchezea visivyo Harry kane na kutoa fursa kwa Spurs kujibu kwa mpigo kwa kufunga mabao mawili ya haraka.

Toby Alderweireld alifunga bao la kwanza la Tottenham kabla ya Harry Kane kufanya mambo kuwa 2-1 .

Lakini Arsenal ilikataa kukubali kushindwa na kusawazisha dakika 14 kabla mchezo kukamilika kupitia Sanchez.