Kiongozi wa Upinzani nchini Sudan afariki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hassan Turabi

Kiongozi wa Upinzani nchini Sudan Hassan Turabi ambaye alimsaidia rais Omar El Bashir kuchukua mamlaka amefariki akiwa na umri wa miaka 84.

Kifo chake kilitangazwa na runinga ya taifa ambayo ilimtaja kuwa muislamu maarufu aliyekuwa na busara.

Ripoti katika mitandao ya kijamii inadai kwamba alifariki hospitalini mjini Khartoum.

Bwana Turabi alikuwa mwandani wa karibu wa rais Omar El Bashir wakati alipochukua mamlaka mwaka 1989 kupitia mapinduzi lakini wakakosana muongo mmoja baadaye.