Benin kumchagua rais mpya

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Thomas Boni Yayi

Raia wa Benin leo wanapiga kura kumchagua mrithi wa rais Thomas Boni Yayi, ambaye amekamilisha mda wake wa mihula miwili.

Uchaguzi huo ulikuwa umeahirishwa kwa mda wa wiki mbili kwa sababu ya kuchelewa kwa zoezi la kuchapishwa na kusambazwa kwa karatasi za kupigia kura.

Haki miliki ya picha
Image caption Bening kumchagua rais mpya

Miongoni mwa viongozi walio mstari wa mbele ni waziri mkuu wa sasa , Lionel Zinsou.

Lakini huku kukiwa na wagombea wengine wapatao 30 kuna dalili uchaguzi huo utaingia duru ya pili.