Brazil: Anayetuhumiwa kwa ufisadi akutana na rais

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Brazil: Anayetuhumiwa kwa ufisadi akutana na rais

Rais wa Brazil Dilma Rousseff amemtembelea rais wa zamani wa nchini hiyo Luiz Inacio Lula da Silva siku moja baada ya bwana Lula kuhojiwa kuhusiana na kashfa ya ufisadi katika kampuni kubwa ya mafuta nchini humo Petrobras.

Dilma na Lula wamejitokeza kwenye roshani ya nje ya jengo la anakoishi Lula kupokea salamu kutoka kwa mamia ya wafuasi wao waliowapungia mkono.

Lula amesema tukio la kumkamata hapo siku ya ijumaa lilinuiwa kumchafulia jina lake na lile la rais wa sasa Bi Rousseff .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lula amesema tukio la kumkamata hapo siku ya ijumaa lilinuiwa kumchafulia jina lake na lile la rais wa sasa Bi Rousseff .

Polisi kwa upande wao wanasema uchunguzi wao unalenga kubaini iwapo viwango vikubwa vya fedha vilivyokuwa vikilipwa katika shirika la kibinafsi la Bw. Lula vinahusiishwa na kashfa hiyo ya ufisadi.

Baadhi ya watu matajiri na wanasiasa mashuhuri nchini Brazil ni miongoni mwa wanaochunguzwa kubaini ushirika wao katika kashfa hiyo ya Petrobras .