Ufisadi: Bilionea wa Iran ahukumiwa kifo

Zanjani
Image caption Babak Zanjani ana utajiri wa utajiri wa $13.5bn

Mfanyabiashara tajiri kupindukia nchini Iran, Babak Zanjani, amepatikana na hatia ya ufisadi, na kuhukumiwa kifo.

Bwana Zanjani alikamatwa mwaka wa 2013, baada ya kutuhumiwa kuwa alichukua dola bilioni moja nukta 9 za pato la taifa, kutokana na mafuta.

Alikanusha tuhuma hizo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Babak Zanjani, amepatikana na hatia ya ufisadi, na kuhukumiwa kifo.

Bw Zanjani alisusiwa na Marekani na Umoja wa Ulaya, kwa kuisaidia serikali ya Iran na kampuni kadha, kuhepa vikwazo vya kiuchumi vya wakati huo, dhidi ya mafuta kutoka Iran.

Alikiri kuwa alitumia kampuni kadha katika Umoja wa Milkia za Kiarabu, Uturuki na Malaysia, kuuza mamilioni ya mapipa ya mafuta ya Iran, kwa niaba ya serikali.

Zanjani anakadiriwa kuwa utajiri wa $13.5bn.

Zanjani alipatikana na hatia ya "ufisadi duniani", moja ya makosa makubwa zaidi katika sheria nchini Iran.

Matajiri wengine wamewahi kunyongwa kutokana na makosa sawa.

Mei 2014, mfanyabiashara tajiri Mahafarid Amir-Khosravi alinyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kupora mabilioni ya dola.