Bomu laua watu 50 Iraq

Haki miliki ya picha AP
Image caption Shambulizi la bomu laua watu 50 Iraq

Takriban watu 50 wameuawa katika mji wa Hillah Iraq baada ya mlipuaji wa kujitolea mhanga kulipua lori lililokuwa limejazwa vilipuzi.

Lori hilo la kubeba mafuta lilisogezwa karibu kabisa na kituo cha kupekulia magari nje ya mji mkuu wa Baghdad kabla ya kujilipua.

39 ya wale waliouawa walikuwa ni raia huku waliosalia wakiwa ni polisi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption 39 ya wale waliouawa walikuwa ni raia huku waliosalia wakiwa ni polisi.

Shambulizi hilo lilitokea mwendo wa saa 9 asubuhi saa za mashariki ya kati.

Watu wengi zaidi walijeruhiwa.

Wakuu wanasema lori lilokuwa na mabomu, liliripuka, na kusababisha vifo, kati ya magari mengi yaliyokuwa yakisubiri kupekuliwa.

Image caption Mji wa Hill uko kilomita mia moja kusini mwa Baghdad.

Mji wa Hill uko kilomita mia moja kusini mwa Baghdad.

Kundi la wapiganaji la Islamic State limedai kutekeleza shambulizi hilo kupitia mtandao wake wa Amaq.