Mwili wapatikana katika lifti siku 30 baadaye

Image caption Apatikana baada ya siku 30 kwenye 'lifti'

Wahandisi wachina wamekuta maiti ya mwanamke ndani ya lifti iliyozimwa ilipopata hitilafu ya nyaya za umeme Xi'an, Uchina.

Inafikiriwa kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 43, alifariki ndani ya lifti hiyo baada ya wahandisi kuzima umeme.

Lifti hiyo ilikuwa na matatizo na hivyo wahandisi wakaitwa.

Hata hivyo inavyoelekea sasa hawakuchukua tahadhari walivyopaswa kabla ya kuzima umeme yapata siku 30 zilizopita.

Image caption Mwanamke apatikana amefariki baada ya lift kuzimwa siku 30 zilizopita

Wahandisi wanasema walipiga kelele kuuliza kama kulikuwepo na mtu ndani ya lifti, kabla ya kukata umeme, kwa sababu kamba ya lifti ilikuwa na kosa, kwenye jumba la makaazi ya watu.

Kwa vile hakuna mtu aliyejibu, walidhani kuwa lifti ilikuwa tupu.

Polisi sasa wamewakamata kwa kukosa kuwajibika ipasavyo na huenda wakawafungulia mashtaka ya kuua bila ya kukusudia.

Image caption Polisi sasa wamewakamata kwa kukosa kuwajibika ipasavyo na huenda wakawafungulia mashtaka ya kuua bila ya kukusudia.

Kutokakana na ukosefu wa marafiki ama hata jamii wa karibu naye hakuna mtu aliyepiga simu ama hata kutoa ripoti kuhusu kukosekana kwake.

Yamkini anadaiwa kuwa ni mtu mpweke.