Magufuli amteua katibu mkuu mpya

Haki miliki ya picha Statehouse Tanzania
Image caption Rais John Pombe Magufuli

Mhandisi John William Kijazi ameteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi nchini Tanzania.

Kabla ya kuteuliwa leo Mhandisi Kijazi alikuwa anahudumu kama balozi wa Tanzania nchini India ambapo majuzi tu alitoa mchango mkubwa katika kuhakikisha wanafunzi raia wa Tanzania wanapata usalama kufuatia shambulizi dhidi ya mmoja wao.

Katika taarifa fupi kutoka kwa ikulu ya rais John Pombe Magufuli Balozi huyo anaanza kazi mara moja.

Mhandisi Kijazi anachukua nafasi iliyowachwa wazi baada ya kuondolewa Balozi Ombeni Sefue.

Haijulikani kwanini balozi Sefue ameondolewa katika wadhfa huo ila taarifa hiyo ya ikulu iliyotiwa sahihi na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa inasema kuwa Sefue atapewa majukumu mengine.