MH-370: Miaka 2 tangu ndege kutoweka

Image caption MH-370: Miaka 2 tangu ndege kutoweka

Ibaada ya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka miwili tangu kutoweka kwa ile ndege ya Malaysia, MH-370 inafanyika nchini humo.

Ndege hiyo ilitoweka kabisa ikiwa na abiria 239 ilipokua safarini kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing Uchina.

Mwaka uliopita,kipande cha mabawa ya ndege hiyo lipatikana ufukweni katika visiwa vya Reunion karibu kilomita 3700 kutoka pale ilipodaiwa kuanguka.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mmoja wa jamaa wa abiria 239 waliotoweka

Licha ya juhudi na operesheni kubwa katika Bahari hindi hakuna chochote kilichopatikana ikiwa ni seghemu kubwa ya ndege ama hata mabaki ya abiria.

Juma lililopita,kipande kingine cha mabaki ya ndege inayoshukiwa kuwa ni ile ya Malaysia M370 ilipatikana karibu na Msumbiji barani Afrika.