Gazeti lililotwaliwa na Uturuki labadilika

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Gazeti lililotwaliwa na Uturuki labadilika

Gazeti la Uturuki lilokuwa la upinzani, Zaman, limechapisha toleo lake la kwanza, tangu kuchukuliwa na serikali.

Msimamo wa gazeti hilo umebadilika sana.

Badala ya malalamiko dhidi ya serikali kwenye ukurasa wake wa kwanza, gazeti la leo, linasifu, moja kati ya miradi mikubwa ya ujenzi ya serikali.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Msimamo wa gazeti hilo umebadilika sana.

Zaman linahusishwa sana na vugu vugu linaloongozwa na shehe anayeishi Marekani.

Vugu vugu ambalo serikali ya Uturuki inaona ni kundi la kigaidi.