Wakuzaji bangi wakutana Israeli

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wakuzaji bangi wakutana Israeli

Wataalamu wanaohusika na matumizi ya bangi kama dawa wanakutana Israel kujadili uvumbuzi zaidi katika kilichokuwa sekta yenye thamani ya mabilioni ya dola duniani.

Hayo ndiyo maazimio ya Canna-Tech inayojumuisha wawekezaji, wakulima halali na watumizi wa bangi kama dawa.

Uwekezaji katika sekta hiyo umekuwa kwa kasi ya juu mno kufuatia uhalalishwa kwa bangi katika majimbo kadhaa nchini Marekani.

Nchini Israeli sekta hiyo ya bangi halali imefunguka na inaelekea kukua kufuatia utafiti na uwekezaji mkubwa.

Afisa mmoja anayesimamia utafiti huo Saul Kaye anasema

''Wagonjwa ni watu wanaopata matibabu ya maradhi ambayo yanapatikana baada ya kutumia kemikali yenye madhara kama vile ugonjwa wa Saratani.

Image caption Nchini Israeli sekta hiyo ya bangi halali imefunguka na inaelekea kukua kufuatia utafiti na uwekezaji mkubwa.

Watu hao ni wale wanaougua ugonjwa wa kusahau, ugonjwa wa Crohn, na wale walio na msongo wa mawazo au mfadhaiko.

Bangi inaweza kusaidia matatizo kama hayo, na bado hatujajua manufaa mengine.

Utafiti unahitajika zaidi, jambo ambalo Israeli inaendelea kuchunguza hasa katika ngazi ya shirikisho

Kwa sasa, kuna utafiti zaidi ya 36 unaoendelea katika hospitali nchini Israeli. ''

Biashara hii ya bangi iliyoanzishwa kwa njia ya soko la magendo, na wafanyibiashara wa awali walitokea hapo.

Lakini kuna kampuni mahususi ya uundaji madawa, katika soko la hisa la Wall Street Marekani sasa yanaangazia biashara ya bangi, hapo ndipo tunaivalia njuga, na bila shaka tunaanza kubadili mtizamo kuhusiana na biashara ya bangi.'' alisema Kaye.