Ubishi wa Messi na Ronaldo wasababisha mauti

Haki miliki ya picha
Image caption Ubishi wa Messi na Ronaldo wasababisha mauti

Polisi nchini India wamemfungulia mashtaka ya mauaji mtu mmoja aliyemdunga kisu rafikiye waliyekosana kuhusu nani kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji bora duniani.

Raia huyo wa Nigeria alimdunga kisu mwezake vilevile mnigeria ambaye walikuwa wakibishana naye.

Inspekta mkuu wa polisi Kiran Kabadi ameiambia shirika la habari la AFP kuwa Michael Chukwuma, 21 ameshtakiwa kwa kuua katika mji wa Mumbai.

Yamkini yeye na mwenzake walianza gumzo kuhusu mchezaji bora katika kitongoji kimoja cha Nallasopara.

Chukwuma na wenzake walikuwa wamemtembelea marehemu kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Raia huyo wa Nigeria alimdunga kisu mwezake vilevile mnigeria ambaye walikuwa wakibishana naye.

''Mmoja wao alikuwa ni shabiki sugu wa mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Messi huku marehemu akimshabikia mfungaji mabao wa Ureno na Real Madrid Ronaldo''.

''Na kwa sababu ambayo haijulikani Chukwuma alimdunga marehemu mwenye umri wa miaka 34 kwa kisu na kumuua papo hapo.'' alisema Inspekta hyo wa Polisi.

Walioshuhudia wanasema kuwa marehemu alimrushia mshukiwa glasi usoni na mshukiwa akamshinda nguvu na kumdunga na ile glasi iliyovunjika, aliongezea Kabadi.