MH-370: Familia zaenda kortini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Familia hizo zinataka fidia na kujua kilichowapata wapendwa wao

Familia 12 za WaChina ambao jamaa zao ni miongoni mwa wale abiria waliotoweka na ile ndege ya Malaysia Mh-370, wamewasilisha kesi mahakamani kudai fidia.

Hatua hiyo imechukuliwa kabla ya mda unaoruhusiwa kufanya hivyo kumalizika hii hapo kesho.

Kwa mujibu wa sheria za kimataifa wanafamilia wana hadi miaka miwili kuwasilisha mahakamani ombi la kutaka fidia tangu kutokea kwa ajali.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption MH-370: Familia zaenda kortini

Licha ya juhudi kubwa za kuitafuta ndege hiyo mpaka sasa haijapatikana.

Katika ombi lao wanafamilia hao wanasema wanataka kujua kilichowasibu jamaa zao.