Mwanahabari azawadiwa $55m na mahakama

Image caption Bi Andrews

Mwanahabari wa michezo nchini Marekani Erin Andrews amezawadiwa dola milioni 55 baada ya kurekodiwa akiwa uchi na mtu aliyekuwa akimfuatilia mienendo yake.

Baada ya siku moja ya majadiliano,baraza la waamuzi lilimpata na hatia ya asilimia 51 mtu huyo,na hivyobasi kuzilazimu hoteli mbili kulipa dola milioni 27.

Bi Andrews ,mwanahabari wa michezo katika kituo cha michezo cha Fox alipigwa picha mwaka 2008 kupitia mwanya wa mlango wa hoteli na Michael David Barret,ambaye aliiweka mtandaoni kanda hiyo ya video.

Alilia wakati uamuzi huo ulipokuwa ukitolewa na kuwakumbatia mawakili wake pamoja na familia yake.

Baadaye katika taarifa iliowekwa katika mtandao wa twitter,aliishukuru mahakama ,na baraza hilo,mawakili na familia yake.