Oromo waandamana Addis Ababa Ethiopia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Oromo waandamana Addis Ababa Ethiopia

Kundi moja dogo la wanafunzi limehusika katika maandamano adimu kuwahi kufanyika katikati ya mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Hii ni kwa mjibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Reuters.

Wanafunzi hao waliandamana dhidi ya hatua ya walinda usalama nchini humo, ambao wanawalaumu kutokana na wimbi la misako, dhidi ya watu wa jamii ya Oromia.

Watu wa jamii hiyo wamekuwa wakiandamana kuopinga hatua ya serikali ya Ethiopia ya kutaka kuwapokonya mashamba yao ilikupanua mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.

Waandamanaji hao wanadai kuwa takriban watu 200 wameuawa au kutoweka tangu maandamano haya ya watu wa Oromo yalipoaanza.

Serikali ya Ethiopia imekanusha madai hayo.

Image caption Jamii ya Oromo ndio iliyokuwa lenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini humo

Shirika la habari la habari la Reuters linasema kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Addis Ababa waliandamana hadi nje ya majengo ya Ubalozi wa Marekani huku wakibeba mabango yenye maandishi:

"Sisi sio magaidi. Acheni kuwaua watu wa jamii ya Oromo''

Kwa mjibu wa takwimu ya hesabu ya raia wa Ethiopia, ya mwaka 2007, Jamii ya Oromo ndio iliyokuwa lenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini humo ikiwa na takriban watu milioni 25 kati ya idadi nzima ya raia nchini humo, iliyofikia milioni 74.