UN: Mkataba wa Ulaya na Uturuki si halali

Haki miliki ya picha .
Image caption UN: Mkataba wa Ulaya na Uturuki si halali

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limeelezea wasiwasi wake kuhusu makubaliano yanayozungumziwa baina ya Umoja wa Ulaya na Uturuki wenye lengo la kuzuia mtiririko wa uhamiaji na wakimbizi kwenda Ulaya.

Image caption Kwa mujibu wa makubaliano baina ya EU na Uturuki, nchi hiyo itawapokea wahamiaji wowote ambao hawatakubaliwa kuingia au kubaki ulaya.

Afisa mkuu wa UNCHR , Filippo Grandi,amekariri kuwa kuwanyima hifadhi wahamiaji na wakimbizi kupitia maamuzi ya kijumla, bila kuangalia maslahi na kwa kusema watarudishwa Uturuki ni kukiuka sheria za kimataifa na hata sheria za Muungano wa Ulaya yenyewe.

Zaidi ya hayo ameelezea kuwa wakimbizi hao si wengi ukilinganisha na uwezo wa mataifa ya Ulaya kukidhi mahitaji hao.

Kwa mujibu wa makubaliano baina ya EU na Uturuki, nchi hiyo itawapokea wahamiaji wowote ambao hawatakubaliwa kuingia au kubaki ulaya.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Zaidi ya hayo ameelezea kuwa wakimbizi hao si wengi ukilinganisha na uwezo wa mataifa ya Ulaya kukidhi mahitaji hao.

Kwa upande wake Uturuki itapewa afueni katika masharti Iliyowekewa nchi hiyo kuhusu maombi yake ya kuwa mwanachama wa EU)