Wanajeshi wa kigeni wavamia al-Shabab

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Haijulikani makanda hao walitoka wapi.

Wanajeshi makamanda wa kigeni wamefanya uvamizi wakitumia ndege aina ya helkopta katika kambi moja ya wanamgambo wa al-shabab karibu na mji ulio kisini mwa Somalia wa Awdhegele.

Wanamgambo hao walifanikiwa kuwatimua lakini wakampoteza mmoja wa wapiganaji wao kwa, mujibu wa msemaji wa al-shabab alipozungumza na shirika la habari la Reuters.

"Walikuwa wamefunika nyuso zao na walizungumza lugha ambayo wapiganaji wetu hawakuielewa. Hatuwafahamu lakinia tulifanikiwa kuwatimua, msemaji huyo alinukuliwa akisema.

Afisa mmoja wa eneo hilo Mohamed Aweys, alithibitisha uvamizi huo uliotokea umbali wa kilomita 50 magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.