Maisha bila ya mitandao ya kijamii

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Mitandao ya kijamii hutumika kwa ukubwa katika maisha ya vijana
Facebook, Snapchat, Instagram, Twitter - mitandao ya kijamii ambayo yamegubika maisha ya watu katika muongo uliopita lakini matumizi yake yametanda kwa ukubwa kiasi cha kuwa kwa baadhi imekuwa ni kama uraibu.

Sasa wanafunzi elfu moja wa Cheshire wanajaribu kubaini maisha yalikuwaje enzi za kabla ya uvumbuzi wa mitandao hiyo ya kijamii.

BBC imewapa changamoto wanafunzi wa shule ya upili ya Tarporley kukaa bila ya kutumia mitandao hiyo kwa wiki moja.

Baadhi ya watu wazima huenda wanaona ni jambo rahisi, kwasababu sio kuwa simu za wanafunzi hao zinachukuliwa, na bado wanaruhusiwa kupiga simu kutuma barua pepe au hata ujumbe mfupi.

Lakini mtihani huu mpaka sasa umedhihirisha jinsi vijana wanavyotegemea sana mitandao hiyo ya kijamii katika maisha yao.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wengi hutazama simu saa zote kuangalia ujumbe kwenye mitandao hiyo

Wanafunzi watatu wanaarifu jinsi mtihani huu ulivyokuwa kwao :

"Fikra ya kuwasiliana moja kwa moja au pengine kusoma kitabu mara nyengine inaonekana kuwa jambo gumu. Ni wengi wanaokiri kucheza michezo katika mitandao lakini kila mtu inaonekana anatumia mitandao ya kijamii kila siku."

Mwalimu mmoja amesema anakaribisha mtihani huo: "mitandao ya kijamii imegubika mno maisha ya watu binafsi, kiasi cha kugeuka kuwa uraibu."

Lakini iwapo umepokonywa njia yako kuu ya kuwasiliana huedna hilo ni tatizo.

Daisy, mwenye umri wa miaka 14, anasema aliupokea mtihani huo vizuri, aligundua kwamba wiki iliopita alitumia saa 16 katika snapchat na ametazamia wiki isiyokuwa na shinikizo la kutaka kuitazama simu yake saa zote.

Lakini mwishoni mwa juma amegundua kuwa hilo sio rahisi:"Ilibidi nizime ujumbe usiingie kwenye simu ili nisishikwe na hamu ya kuitazama simu yangu."

Amegundua mbinu za zamani za mawasiliano kama kutuma barua pepe kwa marafiki walio ng'ambo na pia kupiga simu.

"Sio kuwa ni uraibu, ninaendelea na maisha ya kawaida," anasema Georgia mwenye umri wa miaka 15 kuhusu anavyotumia mitandao ya kijamii.

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Wanafunzi wanajaribu kutambua mbinu mbadala za kuwasiliana

Lakini awali alikuwa na waiwasi kuhusu namna rafiki zake wangellimikiria kwa kuotea tu ghafla kutoka mitandao hiyo.

Kuona ujumbe wa snapchat katika simu yake na kuupuza imekuwa vigumu kwake, lakini: "nimekuwa nikitazama magazeti na majarida," anasema, "na kuzungumzana wazazi wangu kuhusu mambo mengine kando na wao kuwa madereva wangu wa taxi!"

Kati ya wanafunzi hao 1,000 walioanza tihani huo wa kukaa bila ya kutumia mitandao ya kijamii, karibu robo wamekiri kushindwa.

Miongoni mwao ni Sam, alipohitajika kuwasiliana na rafiki yake kucheza tenisi na akagundua hana nambari yake ya simu kumpigia.

Hana nambari ya simu ya mtu yoyote kwenye simu yake, kwa hiyo suluhu ilikuwa ni kutumia snapchat.

Inavyoonekana ni kama wanafunzi wengi watafurahia wakati mtihani huo utakapokamilika ili waweze kurudi katika enzi ya kisasa ya mawasiliano.

Lakini maktaba ya shule ya upili ya Tarporley huenda ingependa mtihani huo uendelee - msimamizi wake anasema hajawahi kushudia idadi kubwa ya vitabu kuombwa kama ilivyokuwa katika wiki iliopita.