Mjukuu wa Mandela aondoshewa kosa la ubakaji

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Inaarifiwa msichana aliyebakwa ni wa miaka 15
Mjukuu wa aliyekuwa rais wa Afrika kusini Nelson Mandela, ameondoshewa kwa muda mashtaka katika mahakama kuu Johannesburg.

Anatuhumiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 15 mwaka jana.

Mamlaka ya kitaifa ya mashtaka imithibitishia BBC kwamba wameondosha mashtaka hayo ya ubakaji kwa muda.

Phindi Louw kutoka mamlaka hiyo NPA amesema ni kutokana na taarifa mpya zilizofichuka na wanahitaji muda zidi kwa uchunguzi.

Mjukuu wa Nelson Mandela ambaye hawezi kutajwa kutokana na sababu za kihseria, ameachiliwa kwa dhamana ya kiasi ya $530 baada ya kuwa kizuizini kwa wiki moja

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 anadaiwa kumbaka msichana huyo katika mgahawa mmoja Johannesburg Agosti 7.

Mshtakiwa amekana mashtaka.

Haki miliki ya picha b
Image caption Nelson Mandela -familia yake imejipata ikiangaziwa na vyombo vya habari

Katika taarifa yake mahakamani amedai kwamba wote waliridhia kitendo hicho na kuwa hakufahamu msichana huyo ni wa chini ya umri wa miaka 18

Amesema mlalamishi alikuwa akinywa pombe na kuvuta sigara kuongezea dhana kwamba ni mtu mzima.

Amesema pia mgahawa huo hauruhusu vijana wasiozidi umri wa miaka 21.

Upnade wa mashtaka utaamua baadaye iwapo kurudisha mashtaka hayo ya uhalifu au la.