Msichana aliyebakwa India ameaga dunia

Image caption Msichana aliyebakwa India ameaga dunia

Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 15 aliyepata majeraha mabaya sana baada ya kubakwa na kisha kuchomwa moto katika eneo lililoko karibu na mji mkuu wa nchi hiyo New Delhi ameaga dunia.

Police wamemkamata mshukuwa mmoja ambaye anasemekana alikuwa na tabia ya kumwandama andama msichana huyo.

Mwanaume huyo anadaiwa kuwa alikuwa mpenzi wake.

Mshukiwa atakabiliwa na mashtaka ya ubakaji na mauaji .

Madaktari wanasema kuwa msichana huyo aliteketea asilimia 95% ya mwili wake .

Image caption Mshukiwa atakabiliwa na mashtaka ya ubakaji na mauaji .

Wakati huohuo wanaume wawili (dereva na msaidizi wake) wamekamatwa katika mji wa Bareilly baada ya kumbaka abiria mmoja ambaye alimdondosha mwanaye na akafa katika mshikemshike hiyo.

Mjadala mkuu kuhusu ongezeko la visa vya ubakaji nchini India umezuka upya badaa ya hasira iliyotokana na kile kisa cha miaka mitatu iliyopita ambapo msichana mmoja mwanafunzi alibakwa na wanaume kadhaa alipokuwa ameabiri basi kuelekea nyumbani .