Ofisi za mawakili wa Mbabazi zavamiwa UG

Image caption Aliyekuwa mgombea urais Uganda Amama Mbabazi
Ofisi mbili za mawakili wanaomuakilisha aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi katika kesi yake kupinga ushindi wa rais Yoweri Museveni katika uchaguzi uliomalizika zimeteketezwa.

Shambulio hilo limetokea usiku.

Mohamed Mbabazi, wakili anayeongoza mawakili wengine katika kesi hiyo ya Mbabazi, amesema vipakatilishi, tarakilishi na nyaraka zilichukuliwa kutoka ofisi yake.

Afisa mmoja wa ulinzi alipigwa na watu walioivamia ofisi hiyo.

Ofisi nyengine iliyoingiliwa ni ya wakili Fred Muwema.

Polisi Uganda wanasema wanafanya uchunguzi.