Marekani na Uingereza zakosoana

Haki miliki ya picha PA
Image caption Rais Obama na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron

Ikulu ya Marekani imeiambia BBC kuwa Marekani inathamini sana uhusiano wake na Uingereza ,hayo yalisemwa saa chache baada ya Rais Obama kuikosoa vikali sera ya mambo ya nje ya Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron.

Rais Obama aliliambia jarida la "The Atlantic"kuwa Uingereza na Ufaransa walisababisha Libya kufikia katika hali mbaya baada ya majeshi yao kuingilia kati.

Hata hivyo BBC imepokea maelezo mengine kutoka Marekani kupitia msemaji wa Ikulu Ned Price yanayomsifu Cameron kwa uongozi wake wa jumuiya ya kijeshi ya nchi za magharibi NATO.

Mhariri wa BBC America ya kaskazini amesema uongozi wa Obama unaonekana kuwa katika mkanganyiko mkubwa.