Aliyeua shujaa wa ukombozi kuachiwa huru

Haki miliki ya picha
Image caption Chris Hani shujaa wa ukombozi wa Afrika Kusini

Mhamiaji mmoja wa kutoka Poland aliyempiga risasi na kumuua, Chris Hani shujaa wa ukombozi wa Afrika Kusini ataachiwa huru katika muda wa wiki mbili zijazo....

Shujaa Chris Hani alikuwa kiongozi wa chama cha kikomunisti na mkuu wa wapiganiaji uhuru wa kikosi cha 'umkhonto we Sizwe' kilichokuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya sera ya ubaguzi wa rangi wa makaburu wa Afrika Kusini...

Lakini kiongozi huyo Chris Hani aliuawa kwa kupigwa risasi na Janusz Walus katika tukio la mwaka wa 1993 lililoghadhabisha raia weusi wa wa Afrika Kusini .

Janusz Walus, mwenye umri wa miaka 63, alikuwa anatumikia kifungo cha maisha kwa mauaji hayo yaliyoiishtua dunia nzima na karibu yasababishe vita kamili kati ya Waafrika na wazungu wa Afrika Kusini hali iliyoepukwa baada ya marehemu Nelson Mandela kuingilia kati na kuhubiri amani.

Sasa mahakama imeamuru mfungwa Janusz Walus aachiliwe kwa msamaha baada ya kufungwa kwa zaidi ya miaka 23.