Clinton na Sanders wakabiliana Florida

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sanders na Clinton

Wagombea wa urais kupitia chama cha Demokrat nchini Marekani Hillary Clinton na mwenzake Bernie Sanders wamekabiliana vikali kuhusu swala la uhamiaji pamoja na maswala mengine katika mjadala mjini Florida.

Mjadala huo uliokuwa moja kwa moja kupitia runinga mjini Miami ulifanyika siku chache tu kabla ya uteuzi wa jimbo la Florida.

Huku wajumbe 246 wakiwa watapiganiwa na vigogo hao wawili wa chama cha Demokrat jimbo hilo la Kusini ni muhimu sana.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sanders na Clinton katika mjadala

Bwana Sanders alikuwa na ushindi wa kushtukiza katika jimbo la Michigan siku ya jumanne,lakini Hillary Clinton aliongeza uongozi wake kwa kupata ushindi mkubwa katika jimbo la Mississippi.

Katika chama cha Republican mgombea aliye kifua mbele Donald Trump alishinda majimbo matatu zaidi ya Michigan,Mississippi na Hawaii.