Aliyebakwa alipwa fidia Ethiopia

Haki miliki ya picha
Image caption Mwathiriwa huyo alilazimishwa kusaini mkataka wa ndoa kinyume na matakwa yake.

Serikali ya Ethiopia imeamrishwa kumlipa fidia ya dola 150,000 mwanamke mmoja ambaye alibakwa miaka 15 iliyopita.

Wanaume watatu walishtakiwa mwaka 2003 baada ya mwanamke huyo kutekwa nyara na kubakwa na wanaume hao, wakati tofauti akiwa na umri wa miaka 13.

Lakini mahakama ya rufaa imekuwa ikibatilisha hukumu ya wanaume hao ikisema kuwa msichana huyo hakubakwa kwa sababu hakuwa bikira.

Mwathiriwa alilazimishwa kusaini mkataka wa ndoa na kiongozi wa kikundi cha wanaume hao baada ya kuzuiwa kwa mwezi mzima kinyume na matakwa yake.