China yazuia meli za Korea Kaskazini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Meli za ulinzi wa pwani ya China

China imepiga marufuku meli za Korea kaskazini kuingia katika bandari zake kuanzia hivi leo.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa china ameripotiwa kutangaza vikwazo hivyo katika mkutano wa kila mwaka wa maafisa wa chama cha kikomunisti mjini Beijing.

Hatua hiyo inaileta China sambamba na vikwazo vikali vilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini wiki iliyopita.

Haki miliki ya picha
Image caption Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un

Japan nayo imetoa malalamishi kwa korea kaskazini kufuatia hatua yake ya kurusha makombora ya masafa mafupi mashariki mwa pwani ya nchi hiyo.

Siku ya Jumanne kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisema kuwa nchi yake imeunda zana za kinuklia zinazoweza kutundikwa kwenye makombora ya masafa marefu.