Stakhabadhi za IS zanaswa na polisi Ujerumani

Image caption Faili za Islamic State

Maafisa wa polisi wa Ujerumani wanachunguza nakala zinazodaiwa kutambulisha idadi kubwa ya wapiganaji wa Islamic State.

Faili hizo zilizopatikana na vyombo vya habari vya Ujerumani na Uingereza zinasemekana kuwa za maswali yanayowabaini maelfu ya mashabiki wa kundi la Islamic State kutoka mataifa 50.

Nakala hizo zinaorodhesha majina,maeneo wanaoyoishi na nambari za simu za wapiganajai hao.

Haki miliki ya picha
Image caption Wapiganaji wa Islamic State

Maafisa wa Ujerumani wanasema kuwa wanaamini kwamba huenda faili hizo ni za kweli.

Taarifa ya wizara imesema kuwa stakhabadhi hizo zinatoa fursa kuwatambua raia wa Urejumani wanaoshiriki katika maswala ya kigaidi ya kundi la IS.