Marekani ilishirikiana na Somalia kushambulia al-shabab

Haki miliki ya picha AP
Image caption al-shabab

Vikosi vya Marekani vilishirikiana na wanajeshi wa Somalia katika uvamizi wa kambi moja ya wapiganaji wa al-shabab ,maafisa wa Marekani wamesema.

Kundi la al-Shabab awali lilisema kuwa lilitibua shambulio la vikosi vya kigeni, lakini maafisa wa Marekani wanasema kwamba wapiganaji kadhaa wa kundi hilo waliuawa siku ya jumatano.

Mataifa kadhaa yamekuwa yakiunga mkono maafisa wa Somalia katika juhudi zao za kukabiliana na wapiganaji wa al-shabab.

Shambulio hilo linajiri baada ya Marekani kusema kuwa ilitekeleza mashambulio ya angani siku ya Jumamosi katika kambi moja ya mafunzo ya al-shabab.

Al-shabab lilisema kuwa mmoja wa wapiganaji wake walifariki huku maafisa wa Somalia wakisema kuwa idadi ya wapiganaji waliouawa ni 15.