Apatikana na hatia ya kumuiba mtoto

Image caption Celeste Nurse(mwenye nguo nyekundu) ndiye mama wa mtoto aliyeibiwa

Mahakama kuu mjini Cape Town nchini Afrika Kusini imempata na hatia mwanamke mmoja, kwa kumteka nyara mtoto mchanga kutoka hospitali moja karibu miaka 20 iliyopita.

Mtoto huyo anadaiwa kunyakuliwa kutoka kitanda cha mamake siku tatu baada ya kuzaliwa mnamo mwaka 1997.

Mwaka uliopita mtoto huyo aliunganishwa tena na familia yake baada ya kujenga urafiki na msichana mdogo katika shule yao ambaye walifanana sana.

Uchunguzi wa DNA ulithibitisha kuwa wasichana hao walikuwa ni dada wawili. Mwanamke anayeshutumiwa amekanusha kuhusika akisema kuwa alipewa mtoto na mtu mwingine baada ya kupoteza mimba.