Mfuasi wa IS akamatwa na Marekani

Image caption silaha za magaidi

Jeshi la Marekani limethibitisha kuwa vikosi vyake maalumu vimefanikiwa kumkamata mtalaam wa silaha za kikemikali wa kundi la wapiganaji wa Islamic State huko nchini Iraq.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani Peter Cook, amesema kukamatwa kwa Sulayman Daoud Al Al Bakr or Abu Daoud ni kufuatia taarifa za kiintelijensia kuhusiana na kundi hilo na matumizi ya silaha za kikemikali. Amesema kuwa taarifa hizi pia zimewezesha vikosi vya Marekani kufanikisha mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji wa Islamic State. Sulayman Daoud anasemekana kuwa alikuwa mtu wa karibu katika mpango wa matumizi ya silaha za kikemikali ambao ulianzishwa na na Saddam Hussein.