Rais wa Angola kung'atuka mamlakani 2018

Image caption Rais Jose Dos Santos wa Angola

Rais wa Angola Jose Eduardo Dos Santos anasema ana mipango ya kung'atuka mamlakani ifikiapo mwaka 2018 baada ya kuongoza nchi hiyo kwa karibu miaka 40.

Alitangaza hayo kwenye hotuba kwa kamati kuu ya chama tawala cha MPLA ambacho amekiongoza tangu mwaka 1979.

Mwaka wa 2001 bwana Dos Santos alisema kuwa angewania muhula mwingine lakini badala yake akabakia madarakani.

Angola ni ya pili katika kuzalisha mafuta lakini uchumi wake umeathirika pakubwa na kushuka kwa bei za mafuta

Kwa sasa Angola iko kwenye mazungumzo na benki kuu ya dunia na shirika la fedha duniani ili iweze kupewa msaada wa fedha.