Japan yaadhimisha miaka 5 ya Tsunami

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Tsunami Japan

Taifa la Japan linaadhimisha miaka mitano tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi na Tsunami iliosababisha vifo vya watu 18,000 wengine wakiwa hawajulikani waliko.

Waziri mkuu Shinzo Abe na mfalme Akihito wanahudhuria makumbusho ya janga hilo mjini Tokyo na walinyamaza kwa mda ili kutoa heshima kwa wale walioathiriwa.

Ukubwa wa tetemeko hilo la 9.0 katika vipimo vya richa lilipiga ufukwe wa bahari wa taifa hilo na kusababisha maji kujaa hatua iliosababisha uharibifu mkubwa kaskazini mashariki mwa pwani ya taifa hilo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waadhimisha miaka 5 ya Tsunami Japan

Pia mafuriko hayo yalisababisha janga baya la kinyuklia katika kinu cha fukushima Daiichi .Maji yaliingia katika kinu hicho na kuathiri mashine za baridi hatua iliosababisha mmomonyoko.