Msaidizi wa Putin aliuawa na kifaa butu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mikhail Lesin

Maafisa wa Marekani wamesema kwamba afisa mmoja wa Juu wa Urusi aliyepatikana akiwa amefariki dunia ndani ya hoteli moja mjini Washington mwaka jana alikufa kutokana na majeraha ya kichwa yaliyosababishwa na kifaa butu.

Maiti ya Mikhail Lesin ilipatikana hapo mwezi Novemba na polisi hawakutoa taarifa za kilichosababisha kifo chake.

Familia ya marehemu ilisema alikufa kutokana na mshtuko wa moyo.

Bwana Lesin alikua mwandani wa Rais Vladmir Putin na alihusika na juhudi za kukandamiza mashirika huru ya habari ya Urusi.

Pia alikua anachunguzwa na majasusi wa Marekani kwa kushukiwa kuhusika na ulanguzi wa pesa.