Wanajeshi wa Sudan Kusini waliua zaidi ya 60

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Amnesty International insema kuwa watu hao walifungiwa kwenye bohari moja lisilo na dirisha au mianya ya kupitisha hewa

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limelaumu wanajeshi wa serikali ya Sudan Kusini kwa mauaji ya wavulana 60 pamoja na wanaume.

Watu hao walifungiwa kwenye bohari moja lisilo na dirisha au mianya ya kupitisha hewa ambapo walifariki kwa kukosa hewa na joto jingi.

Amnesty International imesema vifo hivyo vilitokea nje ya kanisa katoliki katika mji wa leer Oktoba ya mwaka uliopita. Serikali ya Sudan imekanusha madai hayo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Sudan Kusini

Shirika hilo limeongeza walioshuhudia tukio hilo wamesema waliwasikia wafungwa hao wakilia na kupiga mayoe wakitaka kuondolewa kwenye bohari hilo.

Mashahidi hao waliambia Amnesty International kwamba waathiriwa hao walikua wafanyibiashara na wanafunzi na siyo wapiganaji.

Shirika moja la waangalizi wa vita Sudan Kusini limesema jeshi la serikali lilifahamu kuwepo kwa wafungwa hao ndani ya bohari hilo lakini walipuuza kuwaokoa.