Wapiganaji walibaka badala ya mishahara Sudan K

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi nchini Sudan Kusini

Wapiganaji walio watiifu kwa jeshi la Sudan Kusini wameruhusiwa kuwabaka wanawake badala ya mishahara wakati wa vita dhidi ya waasi,ripoti moja ya Umoja wa Mataifa imesema.

Wachunguzi walibaini kwamba wanawake 1,300 walibakwa mwaka uliopita katika jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Unity State pekee.

Katika ripoti tofauti,shirika la Amnesty International linasema kuwa zaidi ya wanaume 60 na wavulana walitiwa ndani ya kasha na kunyimwa hewa na vikosi vya serikali.

Serikali imekana kwamba jeshi lake liliwalenga raia lakini limesema linachunguza.

''Tuna sheria ambazo tunazifuata'',msemaji wa rais Salva Kiir,Ateny Wek Ateny alikiambia kipindi cha BBC Newsday.