Rais wa Brazil akataa kujiuzulu

Haki miliki ya picha Ricardo Stuckert Instituto Lula
Image caption Lula da Silva na Dilma Rousseff

Rais wa Brazil,Dilma Rousseff amesisitiza kuwa hatojiuzulu kutokana na vile alivyouangazia uchumi wa taifa hilo baada ya hatua za kutaka kumshtaki.

Aliwashtumu wapinzani wake kwa kuzua mgogoro wa kisiasa ambao anasema umeharibu uchumi wa taifa hilo.

Bi Rousseff pia alimtetea mtangulizi wake Luiz Lula da Silva kuhusu madai ya ulanguzi wa fedha.

Alisema kuwa hatua ya waendesha mashtaka kutaka kumzuia ni kinyume cha sheria.

Mgogoro huo umesababisha mfumuko mbaya zaidi nchini Brazil,ambalo ndio taifa lenye uchumi mkubwa kusini mwa Marekani.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Dilma Rousseff wa Brazil

Bi Roussef alisistiza kuwa alichaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na hana mpango wowote kuondoka mamlakani.

Kiongozi huyo wa chama cha wafanyikazi pia amekuwa akipata shinikizo kubwa katika miezi ya hivi karibuni kuhusu uchunguzi wa ufisadi inaoshirikishwa na kampuni kubwa ya mafuta ya Petrobas.