Serikali ya Iraq yahimizwa kutekeleza ahadi zake

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption moqtada al sadr

Kiongozi mmoja wa Washia nchini Iraq, Moqtada al Sadr, amezidi kuichagiza serikali kutekeleza mabadiliko ya kisiasa iliyoahidi.

Bwana Sadr ametoa wito kwa wafuasi wake kuanza maandamano Ijumaa ijayo, kwa kukalia pahala pa kuingia katika eneo la Baghdad lisilotakiwa kuwa na mapigano.

Mwezi uliopita, Bwana Sadr alimpa waziri mkuu, Haider al-Abadi, siku 45 kutekeleza ahadi za kuleta mabadiliko hasa kuhusu ufisadi la sivyo bunge litapiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Bwana Sadr ambaye anatoka katika familia maarufu ya viongozi wa Kishia, alipata umaarufu akio-ngoza kundi lenye nguvu la wanamgambo wa Kishia, ambalo lilipambana na wanajeshi wa Marekani, wakati majeshi ya ushirika yakiongozwa na Marekani, yalipovamia Iraq mwaka wa 2003.