UN:Walinda amani wanyanyasaji mashakani

Image caption Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza limepitisha azimio la kusuluhisha suala la unyanyasaji ya kingono unaofanywa na walinda amani wa Umoja huo.

Azimio hilo ni chini ya mpango uliopendekezwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ambapo jeshi au polisi wataondolewa kutoka maeneo ambapo kuna ushahidi wa kuwepo vitendo kama hivyo.

Wanachama 14 wa baraza la ulinzi walipiga kura kuunga mkono azimio hilo isipokuwa Misri ambayo pendekezo lake la kutaka azimio hilo kufanyiwa marekebisho lilikataliwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Walinda amani wa Umoja wa Mataifa

Azimio hilo la Umoja wa Mataifa linafuatia tuhuma zinazowakumba wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kote duniani.