Germanwings: Madaktari watoe siri za marubani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Germanwings: Madaktari watoe siri za marubani

Wachunguzi kutoka Ufaransa, wamependekeza sheria kali inayozuia madaktari kufichua siri za marubani wagonjwa iondolewe.

Wanasema iwapo sheria hiyo isingelikuwepo , ajali iliyosababishwa na rubani mwenza aliyekuwa amezongwa na mawazo isingelitokea.

Wachunguzi hao pia wanasema haifai kuwa marubani wanaruhusiwa wenyewe kujitathmini hali yao ya kiafya.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Abiria wote 150 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, iliyokuwa ikitokea Barcelona kuelekea Dusseldorf Nchini Ujerumani, waliangamia

Wachunguzi hao walitoa mapendekezo hayo katika ripoti yao ya mwisho kuhusiana na ile ajali mbaya ya ndege ya shirika la ndege la Germanwings, iliyoangushwa makusudi na rubani mwenza katika milima ya Alps.

Wanatarajiwa kutoa baadhi ya mapendekezo waliyopata kutoka kwa data ya kifaa cha kurekodi sauti ya ndege hiyo.

Ripoti hiyo ni pamoja na hali ya kiakili ya rubani huyo na usalama wa chumba cha rubani pamoja na hali ya kiafya ya marubani.

Haki miliki ya picha Andreas Lubitz
Image caption Rubani msaidizi, Andreas Lubitz, aliangusha makusudi ndege hiyo kwenye milima ya Alps.

Abiria wote 150 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, iliyokuwa ikitokea Barcelona kuelekea Dusseldorf Nchini Ujerumani, waliangamia.

Rubani msaidizi, Andreas Lubitz, aliangusha makusudi ndege hiyo kwenye milima ya Alps.

Ilifahamika baadaye kuwa Lubitz alikuwa na msongo wa mawazo, baada ya kukosana na mpenziwe wa kike, lakini sheria za kisiri za Ujerumani zinazuia madaktari kutoa siri za ugonjwa wa wateja kwa waajiri.