Merkel akabiliwa na upinzani Ujerumani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bi Angela Merkel

Majimbo matatu ya Ujerumani yanafanya uchaguzi wa serikali za mitaa

Raia hao wanapiga kura za kikanda leo Jumapili

Shughuli hizo za upigaji kura huo zitakuwa ni mtihani mkubwa kwa Merkel kutokana na hatua za kuunga mkono mikakati na sera za wakimbizi.

Mwaka jana, zaidi ya watu milioni moja wakimbizi, waliomba ruhusa ya kuishi nchini Ujerumani.

Lakini katika miezi ya hivi karibuni kumeshuhudia pingamizi dhidi ya hatua Bi Merkel kuhusiana na uamuzi wa kuwakubalia watu wanaokimbia mapigano nchini Syria kuingia nchini Ujerumani.

Image caption Kura za maoni zinaonesha kuwa chama chake cha CDU, huenda kikapoteza kura, ambazo huenda zikanufaisha chama kinachopinga wageni cha (AfD)

Kura za maoni zinaonesha kuwa chama chake cha CDU, huenda kikapoteza kura, ambazo huenda zikanufaisha chama kinachopinga wageni cha (AfD).

Chama cha AfD, kinatarajiwa kupata kura nyingi katika jimbo maskini la mashariki mwa Ujerumani, Saxony-Anhalt.

Uchaguzi huo unafanyika katika majimbo matatu ya Rhineland Palatinate, Baden Wurttemberg na Saxony-Anhalt.