Israel yataka Iran iadhibiwe

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Israel yataka Iran iadhibiwe kwa kufanyia majaribio silaha zake

Waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu ameziomba mataifa yenye nguvu duniani, kuiadhibu Iran kwa hatua yake ya juma lililopita la kufanyia majaribio zana zake za kitonoradi.

Taarifa kutoka kwa afisi ya Benjamin Netanyahu, imewaamuru wanadiplomasia kuelezea swala hilo katika kikao cha mataifa matano yenye nguvu duniani.

Netanyahu anasema mataifa hayo yanapaswa kukumbushwa kuhusiana na majadiliano walioafikiana mwaka jana kuhusiana na mpango wa kinyuklia wa Iran.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tehran inasema kuwa mzinga wake huo ulio na uwezo wa kufika Israeli, haujakiuka kwa vyovyote muafaka uliokubaliwa wa kinyuklia.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa, majibu yao yanafaa kujumuisha nguvu zao za kutaka makubaliano hayo yatekelezwe kama yalivyoafikiwa.

Marekani imesema kuwa itaibua swala hilo katika mkutano wa baraza la umoja wa mataifa hapo kesho Jumatatu.

Tehran inasema kuwa mzinga wake huo ulio na uwezo wa kufika Israeli, haujakiuka kwa vyovyote muafaka uliokubaliwa wa kinyuklia.