Mlipuko mkubwa waua watu 27 Uturuki

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mlipuko mkubwa waua 27 katika kituo cha mabasi Uturuki

Kumetokea mlipuko mkubwa katikati ya mji mkuu wa Uturuki, Ankara.

Afisa muandamizi wa usalama, anasema kuwa takriban watu 27 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Maafisa wa usalama wanakisia idadi ya wale waliojeruhiwa kuwa ni 75.

Haki miliki ya picha DHA
Image caption Madhara ya mlipuko katika kituo cha basi cha Ankara

Mlipuko huo uliwasha moto magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu na kituo kikubwa cha mabasi na bustani katika mtaa wa Kizilay.

Vyombo vya habari vya Uturuki vinasema mlipuko ulitokana na bomu lilotegwa kwenye gari.

Mwezi uliopita, Ankara ilishambuliwa kwa bomu lilouwa karibu watu 30.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwezi uliopita, Ankara ilishambuliwa kwa bomu lilouwa karibu watu 30.

Maafisa wakuu wa Uturuki wakati huo, waliwalaumu wapiganaji wa KiKurd.